Sunday, February 2, 2014

MENEJA WA HABARI MAALUM FM AWATAKA WASIKILIZAJI WA HABARI MAALUM FM KUENDELEA KUWA WAVUMILIVU

                                                    Daniel Magulu Fm Manager Habari Maalum Fm
Meneja wa habari maalum |Fm Daniel Magulu amewataka wasikilizaji wa 97.7
habari maalum Fm kuwa wavumilivu kwasababu vitu vizuri vinakuja kupitia radio
yao hii ni baada ya wasikilizaji wengi kuulizia Radio itaanza lini rasmi baada ya
kuwa kwenye majaribio zaidi ya miezi 6 sasa
Magulu alikaririwa na mwandishi wetu hivi karibuni akiwa ofisini kwake
kuwa bado hawajapata kibari cha kuanza kurusha matangazo kutoka TCRA hivyo
amewataka wasikilizaji wa 97.7 kuendelea kuwa wavumulivu lakini pia waendelee
kuitegea 97.7 Habari Maalum Fm kila wakati.


Tuesday, March 5, 2013

Uchaguzi wa Kenya: Matukio

                                   wa kenya wakiwa kwenye foleni kusubiri kupiga kura

                                         baada ya kula jamaa anashangilia kufanya jambo la msingi
                                                  la kuikomboa inchi yake
                                                          watu wakiendelea kupiga kura

Monday, October 1, 2012

KONGAMANO KUBWA LA VIJANA LILOPEWA JINA LA CALL TO HIGHER DIMENSION KUFANYIKA JMOSI HII




  1. Kanisa la Word Alive Sinza linaloongozwa na Askofu Deogratius Lubala lililoko Sinza Mori jijini Dar es salaam, limeandaa kongamano la kipekee la siku mbili litakalowahusisha vijana kutoka sehemu mbalimbali. Kwa mujibu wa waandaaji wa Kongamano hilo, kongamano hilo litafanyika jumamosi ijayo na jumapili (Tarehe6-7/10/2012) kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi na moja jioni ambapo chakula kitatolewa bure.Siku ya Jumapili kuanzia saa tisa mchana Kongamano litamalizika kwa IBADA KUBWA ya kusifu na kuabudu.

    Kongamano hilo la vijana litakuwa likifanyika kila mwaka na kwa mwaka huu limebeba ujumbe usemao “CALL TO HIGHER DIMENSION”.Vikundi mbalimbali vya uimbaji vitahudumu vikiongozwa na Word Alive Praise Team.Kwa kijana yeyote ambaye ni mkazi wa jiji la Dar es Salaam hii si ya kukosa ukizingatia waalimu watakaohudumu Mungu ameweka hazina kubwa ndani yao kwa utukufu wa wake.Lets meet Sinza Mori jumamosi na jumapili.

    1.Rose Mushi
    2.Pastor Isaack Mallonga
    3.Pastor Daniel Musokwa
    4.Lilian Modesta Mahiga
    5.Pastor Deogratius Lubal 6.Ramsey Ngwelleja

Wednesday, September 26, 2012

SEMINA YA NENO LA MUNGU INAYOENDELEA VIWANJA VYA JANGWANI NA MTUMISH WA MUNGU MWL CHRISTOPHER MWAKASEGE

 Ikiwa ni siku ya nne ya semina ya neno la Mungu inayoendelea katika viwanja vya jangwani Dar es salaam
mtumishi wa Mungu Mwakasege anaendelea kukukaribisha kuja kijifunza neno la Mungu na kupokea muujiza wako , anaendelea kuwa karibisha wakazi wote wa Dar lakini pia unaweza kuungana nae popote pale ulipo duniani kupitia radio na website hizo hapo chini ,
 !!Karibu ujiunge nasi kusikiliza neno la Mungu inayoendelea hapa jijini Dar es salaam kupitia redio wapo,redio sauti ya injili,redio upendo,www.mwakasege.org,www.kicheko.com na www.sautiyainjili.org.Semina itarushwa live kwanzia saa kumi hadi saa kumi na mbili jioni,kwanzia tarehe 23 September 2012 hadi jumapili tarehe 30 september 2012.Mwambie na mwenzako!Mungu awabariki!!

Saturday, August 25, 2012

SENSA KWA MAENDELEO JIANDAE KUHESABIWA KUANZIA USIKU WA LEO

Senhi sa ya watu na makazi kwa ajiri ya maendeleo ya nchi na wananchi itaanza
rasmi leo katika maeneo yote ya Tanzania wito wa serikali kwa jamii ni kuwasihi
kutoa ushirikiano ili kuhakikisha wanapata idadi kamili ya wananchi wake lakini
pia na wageni wanaoishi ndani ya Tz.
jamii inaombwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa kukuballi kuhesabiwa mara moja
na pia kutoa idadi ya kweli ili kuhakikisha zoezi hili litakalo dumu ndani ya siku  saba
kufanikiwa na bila kuwa na vipingamizi vyovyote.
pia serikali inatoa wito kwa viongozi wa dini kuwahamasisha waumini wao kushiriki
katika zoezi zima lakuhesabiwa na bila kuhusisha imani za kidini katika zoezi hili.

Wednesday, August 22, 2012

SENSA YA WATU TANZANIA USIKU WA TAR 25 KUAMKIA 26

Je Utamjuaje Karani wa sensa? Karani wa sensa atafika katika eneo la kuhesabiwa watu akiwa na kitambilisho na atakuwa amevaa sare maalum zitakazomtambulisha. Vile vile atakuwa ameongozana na kiongozi wa eneo unaloishi.