Monday, October 1, 2012

KONGAMANO KUBWA LA VIJANA LILOPEWA JINA LA CALL TO HIGHER DIMENSION KUFANYIKA JMOSI HII




  1. Kanisa la Word Alive Sinza linaloongozwa na Askofu Deogratius Lubala lililoko Sinza Mori jijini Dar es salaam, limeandaa kongamano la kipekee la siku mbili litakalowahusisha vijana kutoka sehemu mbalimbali. Kwa mujibu wa waandaaji wa Kongamano hilo, kongamano hilo litafanyika jumamosi ijayo na jumapili (Tarehe6-7/10/2012) kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi na moja jioni ambapo chakula kitatolewa bure.Siku ya Jumapili kuanzia saa tisa mchana Kongamano litamalizika kwa IBADA KUBWA ya kusifu na kuabudu.

    Kongamano hilo la vijana litakuwa likifanyika kila mwaka na kwa mwaka huu limebeba ujumbe usemao “CALL TO HIGHER DIMENSION”.Vikundi mbalimbali vya uimbaji vitahudumu vikiongozwa na Word Alive Praise Team.Kwa kijana yeyote ambaye ni mkazi wa jiji la Dar es Salaam hii si ya kukosa ukizingatia waalimu watakaohudumu Mungu ameweka hazina kubwa ndani yao kwa utukufu wa wake.Lets meet Sinza Mori jumamosi na jumapili.

    1.Rose Mushi
    2.Pastor Isaack Mallonga
    3.Pastor Daniel Musokwa
    4.Lilian Modesta Mahiga
    5.Pastor Deogratius Lubal 6.Ramsey Ngwelleja

No comments:

Post a Comment