Thursday, June 21, 2012

LIVING GOSPEL MINISTRY:                                  Stand Up Gospel C...

LIVING GOSPEL MINISTRY:                                  Stand Up Gospel C...:                                  Stand Up Gospel Comedy ndani ya City Christian Centre jumapili hii  The King of Stand up Gospel Comedy..
The King of Stand up Gospel Comedy in Tanzania Prezo Chavala akiwa katika moja ya harakati on stage

Baada ya kufanya Tamasha la KUCHEKA TENA la mwisho pale Landmark Hotel,Ubungo mwezi wa tatu na hatimaye Arusha mwanzoni mwa June hatimaye mkali na muasisi wa christian comedy nchini Tanzania anatua tena jijini Dar es salaam kwa Tamasha lake la nne toka ameanza mwishoni mwa mwaka jana pale Ubungo plaza.

Yaani ni kucheka na kucheka na kucheka tena huku ukimsifu Mungu na kujifunza yapasayo kutenda katika maisha yako ya utauwa.Tamasha hili litawasimamisha Up Coming Comedians wa kutosha katika segment maalum ya OPEN MIC, na wale ambao wamezoeleka kama Richard Chidundo,Gerald Mrema,Josephine na wengine watakuwa sambamba na waimbaji kama

Sarah Shila,
Deogratius, Meshack,
Gee & Seth,
WordAlive
Dar es salaam Gospel Bands,
Golden Eagles and
1st Q dance groups

Tamasha Hilo Litaanza Saa 9:00jion-1:30 Usiku
Ukumbi:City Christian Centre(CCC)
Kiingilio 5000/=
Na 2000/= Tu Kwa Watoto.

Katika SERIES hii bado tuko Msimu(SEASON) wa kwanza na hili Tamasha lijalo litakuwa Tamasha la tatu kwa Dar es salaam na ni Episode II. Kama ilivyotaarifiwa mapema Tamasha hili la jpili ijayo(24th June 2012) pamoja na mawili yafuatayo kwa hapa Dar(Yaani Tar 23th Sept na 23/30th Novemba-mkesha wa mwisho) yatafanyika katikaukumbi wa CITY CHRISTIAN CENTRE-UPANGA(Mkabala na Mzumbe Dsm)

Tamasha Hili Limedhaminiwa na Great Potentials Ltd,City Christian Centre(Ccc),TouchingVision,Author2readers,Wordalive Church,Olympus Computers And Chavala Ideas Platform.





Hatimaye kamati inayoandaa tuzo za Muziki wa Injili barani afrika siku ya jana imetoa orodha ya wanamuziki ambao watakuwa wakichuana katika kutafuta washindi wa Kategori mbalimbali.Kwa mujibu wa kamati hiyo mwanamuziki nguli kutoka Tanzania Mwanamama Christina Shusho amefanikiwa kuwa mwanamuziki PEKEE kutoka Tanzania aliyechaguliwa kuingia katika tuzo hizo mwaka huu na ameibuka katika kategori mbili ambazo ni Mwamamuziki bora wa Afrika Mashariki pamoja na mwanamuzik bora wa Kike Barani Afrika.

Christina Shusho, mwaka jana aliingia katika kategori ya mwanamuziki bora wa Afrika mashariki lakini hakufanikiwa kuingia kuibuka mshindi huku mwanadada Emmy Kosgei kutoka Kenya akichukua ushindi katika kategori hiyo.Tofauti na nchi nyingine za Afrika mashariki, kenya imetoa washindani wengi katika kategori mbalimbali.Kategori zinazoonekana kuwa na mpambano mkali ni pamoja na Mwanamuziki bora wa kike na wa kiume barani afrika,Album bora barani Afrika,na mwanamuziki bora kutoa nchi za kusini mwa Afrika ambapo kuna members wa Joyous celebration wakichuana na nguli wengine wa nchi hiyo.Tuzo hizi zinararajiwa kufanyika tar 7 July jijini London nchini Uingereza.


FEMALE ARTIST OF THE YEAR
Kefee -Nigeria
Onos Ariyo- Nigeria
Emmy Kosgei-Kenya
Dena Mwana – Congo
Ntokozo Mbambo- South Africa
Rebecca- UK
Gifty Osei- Ghana
Diana Hamilton-UK
Christina Shusho -Tanzania
Lara George- Nigeria


ARTIST OF THE YEAR- EAST AFRICA
Eko Dydda- Kenya
Emmy Kosgei - Kenya
Exodus- Uganda
Christina Shusho- Tanzania
Lam Lungwar- South Sudan
Sarah K- Kenya
Dawit Getachew-Ethiopia
Kambua-Kenya
Willie Paul- Kenya
Ann Marie Mutesi - Burundi

ALBUM OF THE YEAR
Blessing-Diana Hamilton (UK)
Ololo - Emmy Kosgei (Kenya)
Skuulfoo- Chapter 1 (Ghana)
Colours of Africa- Sonnie Badu (UK)
Crown Him King-Israel Mosehla (South Africa)
Mwamba Mwamba- Solly Mahlangu (South Africa)
Declaring his Name- Muyiwa and Riversongz (UK)
Overflo- Florocka (Akinwunmi Nathan Akiremi) (Nigeria)
Prophecy-Ohemaa Mercy (Ghana)
I Believe – Rebecca (UK)


                                                                                                                                                                MWNJILISTI Kabula George, anatarajia kugawa DVD za albamu ya Nitang’ara Tu kwa kila mtu atakayeingia kwenye Ukumbi wa kanisa la TAG Magomeni Mikumi Julai 8, mwaka huu wakati wa uzinduzi wake.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, Mwinjilisti Kabula alisema ameamu kuweka utaratibu huo, ili kila mtu atakayeingia ukumbini humo aondoke na DVD kwa kuchangia kiasi cha sh. 5,000.

Mwinjilisti Kabula alisema tayari DVD hizo tayari zinapatikana katika maduka mbalimbali yaliyoteuliwa jijini Dar es Salaam.

DVD hizo pia zinapatikana katika mikoa mbalimbali ukiwemo Mwanza, Arusha, Dodoma na Kahama mjini.

Amewataka mashabiki wake kununua DVD halisi ili wanufaike na ubora wa nyimbo hizo, ambazo zinamafundisho kwa kila anayeziangalia

Saturday, June 16, 2012

 Mtumishi wa Mungu johannes akihubiri

 Sherehe hizo za Ishara na miujiza zinaendelea leo njoo wewe walete na wengine walete wagonjwa na wenye shida mbalimbali mungu atawafungua. sherehe hizo zinatarajiwa kuisha Jumapili usitamani kukosa. vilevile mahubiri hayo yanrushwa moja kwa moja na redio wapo unaweza kusikiliza popte ulipo duniani

LIVING GOSPER MINISTRY:

LIVING GOSPER MINISTRY: viva shusho viva

LIVING GOSPER MINISTRY:

LIVING GOSPER MINISTRY:

LIVING GOSPER MINISTRY: Breaking News Tamasha la Injili La Dar Live Laota ...

LIVING GOSPER MINISTRY: Breaking News Tamasha la Injili La Dar Live Laota ...: Breaking News Tamasha la Injili La Dar Live Laota Mbawa Habari za Uhakika Blog hii iliyozipata punde baada ya kuwasiliana na Waandaaji na Wa...
Breaking News Tamasha la Injili La Dar Live Laota Mbawa
Habari za Uhakika Blog hii iliyozipata punde baada ya kuwasiliana na Waandaaji na Washiriki wa Tamasha hilo wamethibitisha kuwa Tamasha hilo "imeota mbawa" halipo tena siku ya Jumapili Mpaka wakati litakapotangazwa tena.


Blog ilipotaka kufahamu ni kwanini Tamasha hilo lilo limehairishwa dakika za mwishoni, wahusika hawakuwa tayari kuliweka bayana zaidi ya kueleza kuwa "taratibu zilikuwa hazijakamilika"


Tamasha hili lilozua mjadala siku ya leo katika Mitandao Ya Kijamii ambayo blog hii imetupia kwenye Blog lilikuwa likijumuisha wanamuziki Christina Shusho, Upendo Nkone, Martha Mwaipaja, Faraja, Sarah Mvungi na Kabula John limesogezwa mbele mpaka taratibu za ndani zitakapokuwa zimekamilika.