Wednesday, September 26, 2012

SEMINA YA NENO LA MUNGU INAYOENDELEA VIWANJA VYA JANGWANI NA MTUMISH WA MUNGU MWL CHRISTOPHER MWAKASEGE

 Ikiwa ni siku ya nne ya semina ya neno la Mungu inayoendelea katika viwanja vya jangwani Dar es salaam
mtumishi wa Mungu Mwakasege anaendelea kukukaribisha kuja kijifunza neno la Mungu na kupokea muujiza wako , anaendelea kuwa karibisha wakazi wote wa Dar lakini pia unaweza kuungana nae popote pale ulipo duniani kupitia radio na website hizo hapo chini ,
 !!Karibu ujiunge nasi kusikiliza neno la Mungu inayoendelea hapa jijini Dar es salaam kupitia redio wapo,redio sauti ya injili,redio upendo,www.mwakasege.org,www.kicheko.com na www.sautiyainjili.org.Semina itarushwa live kwanzia saa kumi hadi saa kumi na mbili jioni,kwanzia tarehe 23 September 2012 hadi jumapili tarehe 30 september 2012.Mwambie na mwenzako!Mungu awabariki!!

Saturday, August 25, 2012

SENSA KWA MAENDELEO JIANDAE KUHESABIWA KUANZIA USIKU WA LEO

Senhi sa ya watu na makazi kwa ajiri ya maendeleo ya nchi na wananchi itaanza
rasmi leo katika maeneo yote ya Tanzania wito wa serikali kwa jamii ni kuwasihi
kutoa ushirikiano ili kuhakikisha wanapata idadi kamili ya wananchi wake lakini
pia na wageni wanaoishi ndani ya Tz.
jamii inaombwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa kukuballi kuhesabiwa mara moja
na pia kutoa idadi ya kweli ili kuhakikisha zoezi hili litakalo dumu ndani ya siku  saba
kufanikiwa na bila kuwa na vipingamizi vyovyote.
pia serikali inatoa wito kwa viongozi wa dini kuwahamasisha waumini wao kushiriki
katika zoezi zima lakuhesabiwa na bila kuhusisha imani za kidini katika zoezi hili.

Wednesday, August 22, 2012

SENSA YA WATU TANZANIA USIKU WA TAR 25 KUAMKIA 26

Je Utamjuaje Karani wa sensa? Karani wa sensa atafika katika eneo la kuhesabiwa watu akiwa na kitambilisho na atakuwa amevaa sare maalum zitakazomtambulisha. Vile vile atakuwa ameongozana na kiongozi wa eneo unaloishi.

Saturday, August 11, 2012

KWA WAKAZI WA ARUSHA NA VITONGOJI VYAKE

Conference na mkutano mkubwa wa injiri mjini arusha unatarajiwa kufanyika kuanzia
tar 14-19 agosti mwaka huu '

KILICHO JILI LEO KWENYE LOVE TANZANIA FESTIVAL

                                                      Mtumishio wa Mungu Andrew Palau
                            Masanja mkandamizaji akishambulia jukwa la Tanzania Love Festival
          Mwimbaji Don Moen akisifu na kuabudu na umati wa watu waliofika   kwenye viwanja vya Jangwani

Friday, August 3, 2012

MAKANISA 800 KUKUTANA KWA PAMOJA NDANI YA LOVE FESTIVAL TANZANIA


MAKANISA 800 KUKUTANA KWA PAMOJA NDANI YA LOVE FESTIVAL TANZANIA






Miwani 10,000 za kusomea kugawiwa Bure


Wafanyabiashara wakubwa na viongozi wa serikari kuinjilishwa kupitia Evening Dinner


Kikundi maalumu cha Michezo ya Baiskeli kuonyesha ufundi wa kuchezea baiskeli


Tofauti na Donnie Moen, Nicole C Mullen ,Christina Shusho,John Lissu,Pastor Safari Paul wa DPC kuongoza Love Tanzania Festival Praise Team

Love Tanzania Festival ni kusanyiko kubwa la kihistoria litakalofanyika kuanzia tarehe 11-12/08/2012 katika viwanja vya Jangwani kuanzia saa saba mchana mpaka saa 2 Usiku.Kwa mujibu wa mmoja wa waandaaji wa kusanyiko hilo Brother Prosper Mwakitalima ameiambia Hosanna Inc kuwa katika kufanikisha kusanyiko hilo makanisa zaidi ya 800 yameshiriki katika maandalizi ya tukio hilo maalumu lenye lengo la kuwakutanisha watu wa dini,kabila,rika zote kwa lengo la kumtukuza Kristo Yesu.

Kwa mujibu wa Mwakitalima kabla ya shughuli ya tarehe 11 na 12 kuna shughuli mbalimbali ambazo Love Tanzania Festival itakuwa ikizifanya kwa jamii ya Tanzania.

Ifuatayo ni Ratiba ya shughuli nzima za LOVE TANZANIA FESTIVAL.

Tarehe 5 August 7:00 Asubuhi – 10.00 Asubuhi
Mbeba maono wa Love Tanzania Featival mtumishi Andrew Palau atahubiri ibada zote mbili katika kanisa la Upanga City Christian Centre (UCC)

Muimbaji mashuhuri Nicole C Mullen atahudumu

Tarehe 7 August 10 Asubuhi

Kutafanyika Mkutano wa waandishi wa habari(Press Conference) katika Ukumbi wa TBD ambapo Andrew Palau akiambatana na wachungaji, Maaskofu,waimbaji na kikundi cha waonyesha michezo ya Baiskeli watakuwa wakiongea na waandishi wa habari.
Usiku huo wa Tarehe 7 kuanzia saa 11.30 jioni katika ukumbi wa KARIMJEE kutafanyika WOMENS DINNER ambapo kamati imewakaribisha zaidi ya wamama 600 nao watapata nafasi kusikiliza na ya kubadilishana mawazo na Andrew Palau.

Tarehe 8 August 12:00 jioni

Katika Ukumbi wa Karimjee Hall kutafanyika hafla ya chakula cha jioni ambapo viongozi mbalimbali wa serikali na wafanyabiashara wakubwa watapata nafasi ya kukutana na Palau ambapo mtumishi huyo atatumia nafasi hiyo kumtangaza kristo kwa tabaka hilo la watanzania ambao kwa namna moja au nyingine limekuwa ni vigumu kufikiwa na injili ya Yesu kristo.

Tarehe 10:August 8:00 Mchana – 9:00 Jioni

Kutafanyika maozoezi(Rehesal)ya michezo ya Baiskeli ambapo kikundi cha JUNGLE RUSH FMX kutoka Afrika ya Kusini kitakuwa kikifanya mazoezi hayo ili kujiweka sawa.Baada ya mazoezi hayo kutafanyika MAOMBI rasmi kwa ajili ya kuuweka wakfu uwanja wa Jangwani kwa ajili ya shughuli nzima ya tarehe 11-12.



VITUO MAALUMU KWA AJILI YA CLINIC YA MACHO

Love Tanzania Festival siyo tu itahusisha kuponya ROHO za watu kupitia neno la Mungu, pia watakuwepo Madaktari maalumu wa macho kutoka Marekani na watashirikiana na madaktari wa ki-Tanzania ambapo watakuwa wakipima watu mbalimbali wenye matatizo ya macho BURE, wale wenye matatizo ya kutoona vizuri maandishi watapewa MIWANI za kusomea BURE.Jumla ya miwani zipatazo elfu kumi(10,000) zipo kwa ajili ya kugawiwa kwa watanzania ambao watabainika na matatizo hayo, Ratiba ya Clinic hiyo itakayokuwa na vituo vinne ni kama ifuatavyo.

Kituo 1:St Nicholaus Anglican Church –ILALA

Kituo cha 2:Tanzania Assemblies of GOD (TAG-Mbagala)

Kituo cha 3:Lutheran Chuch – Vingunguti

Kituo cha 4: Baptist Mission Church – Magomeni

Kliniki zote hizi zitakuwa zinaanza saa nne asubuhi mpaka saa kumi jioni

Donnie Moen kuhudumu