† Miwani 10,000 za kusomea kugawiwa Bure
† Wafanyabiashara wakubwa na viongozi wa serikari kuinjilishwa kupitia Evening Dinner
† Kikundi maalumu cha Michezo ya Baiskeli kuonyesha ufundi wa kuchezea baiskeli
† Tofauti
na Donnie Moen, Nicole C Mullen ,Christina Shusho,John Lissu,Pastor
Safari Paul wa DPC kuongoza Love Tanzania Festival Praise Team
Love
Tanzania Festival ni kusanyiko kubwa la kihistoria litakalofanyika
kuanzia tarehe 11-12/08/2012 katika viwanja vya Jangwani kuanzia saa
saba mchana mpaka saa 2 Usiku.Kwa mujibu wa mmoja wa waandaaji wa
kusanyiko hilo Brother Prosper Mwakitalima ameiambia Hosanna Inc kuwa
katika kufanikisha kusanyiko hilo makanisa zaidi ya 800 yameshiriki
katika maandalizi ya tukio hilo maalumu lenye lengo la kuwakutanisha
watu wa dini,kabila,rika zote kwa lengo la kumtukuza Kristo Yesu.
Kwa
mujibu wa Mwakitalima kabla ya shughuli ya tarehe 11 na 12 kuna
shughuli mbalimbali ambazo Love Tanzania Festival itakuwa ikizifanya kwa
jamii ya Tanzania.
Ifuatayo ni Ratiba ya shughuli nzima za LOVE TANZANIA FESTIVAL.
Tarehe 5 August 7:00 Asubuhi – 10.00 Asubuhi
Mbeba
maono wa Love Tanzania Featival mtumishi Andrew Palau atahubiri ibada
zote mbili katika kanisa la Upanga City Christian Centre (UCC)
 |
Muimbaji mashuhuri Nicole C Mullen atahudumu
|
Tarehe 7 August 10 Asubuhi
Kutafanyika Mkutano wa waandishi wa habari(Press Conference)
katika Ukumbi wa TBD ambapo Andrew Palau akiambatana na wachungaji,
Maaskofu,waimbaji na kikundi cha waonyesha michezo ya Baiskeli watakuwa
wakiongea na waandishi wa habari.
Usiku
huo wa Tarehe 7 kuanzia saa 11.30 jioni katika ukumbi wa KARIMJEE
kutafanyika WOMENS DINNER ambapo kamati imewakaribisha zaidi ya wamama
600 nao watapata nafasi kusikiliza na ya kubadilishana mawazo na Andrew
Palau.
Tarehe 8 August 12:00 jioni
Katika Ukumbi wa Karimjee Hall kutafanyika hafla ya chakula cha jioni
ambapo viongozi mbalimbali wa serikali na wafanyabiashara wakubwa
watapata nafasi ya kukutana na Palau ambapo mtumishi huyo atatumia
nafasi hiyo kumtangaza kristo kwa tabaka hilo la watanzania ambao kwa
namna moja au nyingine limekuwa ni vigumu kufikiwa na injili ya Yesu
kristo.
Tarehe 10:August 8:00 Mchana – 9:00 Jioni
Kutafanyika
maozoezi(Rehesal)ya michezo ya Baiskeli ambapo kikundi cha JUNGLE RUSH
FMX kutoka Afrika ya Kusini kitakuwa kikifanya mazoezi hayo ili kujiweka
sawa.Baada ya mazoezi hayo kutafanyika MAOMBI rasmi kwa ajili ya
kuuweka wakfu uwanja wa Jangwani kwa ajili ya shughuli nzima ya tarehe
11-12.
VITUO MAALUMU KWA AJILI YA CLINIC YA MACHO
Love
Tanzania Festival siyo tu itahusisha kuponya ROHO za watu kupitia neno
la Mungu, pia watakuwepo Madaktari maalumu wa macho kutoka Marekani na
watashirikiana na madaktari wa ki-Tanzania ambapo watakuwa wakipima watu
mbalimbali wenye matatizo ya macho BURE, wale wenye matatizo ya kutoona
vizuri maandishi watapewa MIWANI za kusomea BURE.Jumla ya miwani
zipatazo elfu kumi(10,000) zipo kwa ajili ya kugawiwa kwa watanzania
ambao watabainika na matatizo hayo, Ratiba ya Clinic hiyo itakayokuwa na
vituo vinne ni kama ifuatavyo.
Kituo 1:St Nicholaus Anglican Church –ILALA
Kituo cha 2:Tanzania Assemblies of GOD (TAG-Mbagala)
Kituo cha 3:Lutheran Chuch – Vingunguti
Kituo cha 4: Baptist Mission Church – Magomeni
Kliniki zote hizi zitakuwa zinaanza saa nne asubuhi mpaka saa kumi jioni
 |
Donnie Moen kuhudumu |